Alhamisi, 31 Julai 2014

Jennifer Mgendi kuja na Mama Mkwe

Mwimbaji nyota wa muziki wa Injili nchini, amekamilisha shughuli ya uchukuaji picha wa filamu yake mpya itakayoenda kwa jina la Mama Mkwe.
Akiongea na safu hii, Jennifer amesema filamu hiyo imekamilika katika hatua zote za utayarishaji na inasubiri kuingia hatua ya uzalishaji na usambazaji.
Akiwataja walioshiriki kucheza filamu hiyo, amesema umewashirikisha wasanii mbalimbali wa maigizo na waimbaji wa muziki wa injili akiwemo Bahati Bukuku, Christine Matai, Godliver Vedastus, Mussa Banzi, Senga, Husna Chobis, Pierre na wengine wengi.
Waongozaji wa filamu hiyo ni Bi Mgeni Khamis na Chrissant Mhengga.
Wadau wote wameombwa kupata nakala halisi